CHUJI AAMUA KULA SAHANI MOJA NA SIMBA


SAKATA la kiungo Athuman Idd 'Chuji' na Simba limechukua sura mpya baada ya mchezaji huyo kudai kuwa atahakikisha Simba haitacheza ligi msimu huu mpaka wamalizane naye. Chuji ambaye tayari amewasilisha suala lake kwenye vyombo vya sheria amesema anashangazwa na kitendo cha viongozi wa Simba kumkana na kudai kuwa walishamalizana naye kitu ambacho si cha kweli.
"Juzi katibu wa Simba (Evodius Mtawala), alinipigia akaniambie nisaini fomu ya kuvunja mkataba ili ionekane kuwa tulielewana na nimeuvunja zamani kitu ambacho sivyo, mimi nimekataa kwa kuwa wanataka kunifanyia uhuni." alisema Chuji
"Wamenipigia kwa vile wamejua wamechemsha, kitendo nitakachowafanyia hawataamini labda wanilipe malipo yangu yote nitahakikisha naisimamisha isicheze Ligi, leseni na mkataba wa kuichezea Simba miaka miwili ninayo,"alisema Chuji ambaye alidai tayari barua ya mwanasheria wake ameifikisha ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania kuishtaki Simba kwa kumpiga danadana mteja wake.
Chuji ameingia kwenye mzozo na uongozi wa klabu hiyo baada ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji chini ya Alex Mgongolwa kubaini kuwa Chuji anamkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi na kwamba timu ya Villa Squard ambayo Chuji alikuwa akifanya mazoezi haijamuombea usajili.
Simba ilitangaza kuvunja mkataba na Chuji kwa madai ya utomvu wa nidhamu na kudai kuwa alikuwa kwenye uangalizi.Mbali na Chuji uongozi wa klabu hiyo pia unatakiwa umlipe mchezaji Meshack Abeil na Mohamed Banka ambao wamekatisha mikataba yao.
Meshack aliiambia Mwananchi jana kuwa Katibu mkuu wa wekundu hao wa Msimbazi alimpigia simu jana kuwa watamalizana naye.
"Katibu kaniambia atanipigia baadae nikachukue malipo yangu, mkataba wangu ni wa mwaka mmoja, wameniharibia nilipata nafasi ya kwenda kucheza Botswana wakakataa kuvunja mkataba wangu mapema ili niwe huru matokeo yake nimekosa ile nafasi wameniharibia maisha yangu nilitakiwa Julai 20 niwe nimesharipoti kule, nawapa leo (jana) na kesho (leo), kama hawatamalizana na mimi naliacha suala hilo kwa wakili wangu Edson

Comments