CHEKA, MAUGO IDDI PILI MORO

Kwa unyofu nawafahamisha kuwa pambano kati ya MADA MAUGO na FRANCIS CHEKA litapiganwa siku ya Idd Pili aidha mabondia hawa watapima uzito mjini Morogoro siku ya Idd Mosi. Pambano hili la uzito wa Super Middle yaani Kgs 76 siyo pambano la ubingwa.awali lilikuwa limepangwa kufanyika katika uzito wa Middle yaani Kgs 73 ambao Francis Cheka alikuwa bingwa wa mabara wa Universal Boxing Organisation ( UBO Intercontinental ).
 Kwa sasa Francis Cheka ameongeza uzito na hivyo hawezi kupigana tena katika uzito wa Middle na UBO tayari wameuchukua bingwa huo na kuutangaza kuwa uko wazi. http://uboboxing.com/champions.htm
 Tanzania imebakia na Mbwana Matumla pekee mwenye ubingwa unaotambuliwa na UBO. Juma Fundi alinyang’anywa ubingwa wa dunia wa UBO wa uzito wa Fly baada ya kudundwa na Nasibu Ramadhan kwenye pambano la ubingwa wa mabara unatambuliwa na World Boxing Forum ( WBForum ).
Iwapo kuna swali basi usisite kuniuliza maana pambano hili limeidhishwa na Shikisho la Masumbwi la Tanzania ( PST ).
Asante,
Emmanuel Mlundwa
0777-635432 na 0754-474719 na 0716-336022 na 0787-518400

Comments