BSS WAIBURUZA MAHAKAMANI AIRTEL

MKURUGENZI WA BENCHMARK PRODUCTION RITHA POULSEN  KULIA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO KUHUSIANA NA SHINDANO LA BONGO STAR SEARCH

WAANDAAJI wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Bongo Stars Search, (BSS), Second Chance 2011 wameishitaki katika Mahakama ya Biashara Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kutokana na kuvunja mkataba wa udhamini wa shindano hilo.

Mkurugenzi wa Benchmark Production, ambao ndio waandaaji wa BSS, Ritha Poulsen, alisema jijini Dar es Salaam  kwamba, mwaka jana waliingia mkataba wa udhamini na kampuni hiyo kwa miaka mitatu, lakini anashangaa mwaka huu wakati shindano limeishaanza, Airtel walitangaza kuvunja mkataba ambao wenyewe waliomba kuwadhamini.
“Yaani kitendo hiki kimetusikitisha sana, kwani ni kama kuharibu biashara ya mtu, kama tungekuwa wepesi na kuvunjika moyo tungeamua kuacha mwaka huu, lakini tulijipa nguvu na kusaka wadhamini wengine na matokeo yake tumefika hapa tulipo,” alisema.
Madam Ritha aliongeza kuwa wameamua kwenda mahakamani kuhakikisha wanapata haki yao ya msingi na hasa ikizingatiwa kuwa, hiyo ni biashara, hivyo si vizuri kuharibiana.

Comments