BOSI LYON APINGANA NA TFF

MMILIKI wa klabu ya African Lyon, Rahim Zamunda amesema uamuzi wa kamati ya katiba,sheria na hadhi kwa wachezaji kuwazuia kufanya usajili wa wachezaji wapya ili kushinikiza kulipwa kwa kiasi cha Sh 8.6 milioni ni uamuzi wa kibabe na hauna nia nzuri ya kuendeleza soka nchini ambapo amesisitiza hawatalipa fedha hizo.

Kamati hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) iliyo chini ya mwanasheria Alex Mgongolwa ilifikia uamuzi wa kuizuia African Lyon kufanya usajili wa wachezaji wapya kupitia kikao chake kilichofanyika jijini Dar es Salaam wiki iliyopita kujadili pingamizi mbalimbali zilizowasilishwa na klabu za Ligi Kuu.
Kamati hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya waliowahi kuwa wachezaji wa klabu hiyo, Godfrey Komba na Abdul Masenga kuwasilisha malalamiko wakidai kuachwa na timu hiyo bila kulipwa haki zao, huku pia Kamati hiyo ikitishia kuiondoa katika orodha ya timu zitakazoshiriki ligi kuu ikiwa haitalipa fedha hizo hadi kufikia Agosti 17.



Comments