BASENA: YANGA HAWANINYIMI USINGIZI

KOCHA wa Simba, Mganda Moses Basena amesema mechi ya watani zao wa jadi Yanga haimpi presha ila anachofikiri ni Ligi Kuu ya Tanzania bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti 20.

Basena amesema hawezi kuumizwa kichwa na mechi moja ya Yanga na kwamba anaandaa wachezaji wake kiushindani ili aweze kutwaa ubingwa wa bara walioupoteza msimu uliopita.
Akizungumza kwa simu, Basena ambaye timu yake imeweka kambi Zanzibar alisema mpaka sasa mazoezi yanaendelea vizuri, wachezaji wake wameanza kumuelewa na kufuata yale anayowafundisha na anaimani kubwa wataleta upinzani mkubwa kwenye ligi.
"Sina wasiwasi na kikosi changu na sikiandai kwa ajili ya mechi ya ngao ya hisani, naangalia mbele zaidi, nadhani kushinda mechi zote za ligi na kutwaa ubingwa ni bora zaidi kuliko kushinda mechi moja tu dhidi ya Yanga, nitafurahi kuona nachukua ubingwa wa Ligi na sio kumfunga Yanga,"alisema Basena.

Comments