BASATA YAPONNGEZA WASHINDI TUZO ZA EMAS

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapongeza wasanii wa Tanzania walioshinda Tuzo za muziki za Afrika Mashariki (EMAS) zilizofanyika jumamosi iliyopita huko Nairobi, Kenya.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Katibu Mkuu wa Basata Ghonche Materego, ilisema kuwa ushindi huo ni heshima kubwa kwa Taifa la Tanzania.
Wasanii wa Tanzania walionyakua tuzo hizo ni pamoja na bendi ya Muziki wa dansi ya Msondo Ngoma, Ambwene Yesaya ‘AY’, Khamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Christina Shusho.
Aidha, Katibu huyo alisema baraza hilo pia linawapongeza wasanii wengine wa Tanzania ambao walipata nafasi ya kuteuliwa kuwania tuzo hizo wakiwemo Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, Vumilia Abraham, Upendo Nkone, kwaya ya Mwanza, Christian Bella, Mabeste, Beatrice Mathew na Tina Mdulule.

Comments