AZAM YAUA, NGASSA, KIPRE TCHETCHE WAPIGA MABAO

TIMU ya Azam imeendelea kutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi kwa kuichapa JKT Ruvu kwa mabao 3-2.

Mshambuliaji Mrisho Ngassa alifunga bao la tik tak dakika 88 na kuipa ushindi huo Azam ambayo ililazimika kusawazisha mara mbili baada ya JKT Ruvu kupata bao la kuongoza dakika 5, kupitia Hussen Bunu na Amos Mgisa (21).
Azam walisawazisha kupitia Kipre Tchetche na John Bocco kabla ya Ibrahimu Shikanda kupiga krosi iliyounganishwa na Ngassa.

Comments

  1. hvi Dina uwanja huu unaitwaje kwani kila siku tunashindwa kuelewa waandishi wangine wanaita Chamazi stadium wangine wanaita Azam stadium na vile vile kama utapata nafasi tunaomba utupigie picha uwanja huo tuone nasi tulio mbali kunazia majukwaa hadi uwanja wenyewe.
    wako
    James
    Hollnd

    ReplyDelete

Post a Comment