AZAM WAPIGWA 'ARBA' UGANDA

AZAM FC, wakiwa kwenye ziara yao nchini Uganda wameanza vibaya baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Bunamwaya mchezo uliochezwa juzi na leo itacheza na Sport Club Villa kwenye Uwanja huo huo wa Nakivumo uliopo jijini Kampala.

Mshambuliaji Hamis Mcha alifunga mabao mawili na Kipre Tchetche alifunga bao kwa Azam iliyokubali kipigo hicho kutoka kwa Bunamwanya timu iliyoonyesha soka safi kwenye fainali za Kombe la Kagame mwaka huu.
Baada ya mchezo huo Azam leo itacheza na Sport Club Villa ukiwa ni mchezo wa pili na kesho itacheza na KCC FC kabla ya kumaliza na Victors FC wenyeji wao Uganda na kuelekea Rwanda kucheza mechi moja dhidi ya Polisi Rwanda Jumanne ya Agosti 16.

Comments