ADEBAYOR ATUA SPURS KWA MKOPO

KLABU ya Tottenham imethibitisha kumsajili mshambuliaji Emmanuel Adebayor kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefukutoka Manchester City. Mapema wiki hii, kocha wa Tottenham, Harry Redknapp alithibitisha klabu hiyo kuwa kwenye mazungumzo na City ili wakopeshwe mshambuliaji huyo wa Togo mwenye umri wa miaka 27. Adebayor alitofautiana na kocha wa Manchester City, Roberto Mancini mwaka jana na akaenda kucheza kwa mkopo Real Madrid.

Comments