YANGA KUMPELEKEA RAIS KIKWETE KOMBE LA KAGAME


YANGA imepanga kulipeleka Kombe la ubingwa wa michuano ya Kagame kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, imefahamika.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa jana na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga, hatua hiyo ni kutokana na ubingwa huo kuwa fahari ya Tanzania bila kujali umetua katika klabu gani, hasa ikizingatiwa michuano hiyo imefanyika kwenye ardhi ya Tanzania.
Nchunga alisema kwa michuano hiyo kufanyika Tanzania iliyo chini ya Rais Kikwete na kombe hilo likabaki nchini, wameona wao Yanga hawana budi kulipeleka taji hilo Ikulu kwani yeye ndie mkuu wa nchi.
Alisema, mbali ya kulipeleka Ikulu, pia wamepanga kulifikisha hadi bungeni mjini Dodoma kwa lengo la kutoa fursa kwa wabunge ambao kimsingi ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo mbalimbali,  kulishuhudia kombe hilo.
Nchunga alisema, kwa mazingira hayo ndiyo maana wao Yanga wamepokea salamu kutoka bungeni Dodoma, hivyo kwa heshima na kutambua umuhimu na thamani ya chombo hicho kwa maendeleo ya nchi, wameamua kuwapelekea kombe hilo.
“Tumepokea salamu za pongezi toka bungeni na tunaahidi kulipeleka kombe bungeni ili wabunge wapate na wao kulishuhudia na hata kulishika,” alisema.
Nchunga aliongeza kuwa, mbali na sehemu hizo wanatarajia pia kulipeleka kombe hilo  baadhi ya sehemu ili kuwapa fursa mashabiki wao walioko kila kona ya nchi kulishuhudia.                                                        

Comments

  1. SAFI SAAAAANA MPELEKEEENI KOMBE HILO ALIONE NA KWAMBA WATU WAJUWE SISI NDIYO SELIKALI YANGA OYEEE TIL I DIE,,,,


    REV.J
    USA

    ReplyDelete

Post a Comment