WAREMBO 30 KUSHIRIKI MISS TANZANIA 2011

PRESS RELEASE MISS TANZANIA 2011
26TH July 2011
WANYANGE 27 kutoka katika kanda 10 za Tanzania Bara, wamepata tiketi ya kushiriki fainali za Vodacom Miss Tanzania 2011, zinazotarajia kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika sehemu itakayotangazwa baadaye na Kamati ya Miss Tanzania.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugezni wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga, alisema mashindano ya mwaka huu kuanzia ngazi ya vituo hadi kanda, yameonekana kuwa na mvuto mkubwa tofauti na miaka mitatu iliyopita.
“Washiriki wengi wamejitokeza mwaka huu, tofauti na miaka mitatu iliyopita na pia mwamko nao umeongezeka ambapo hata wadhuriaji wamejitokeza kwa wingi  na kuweka rekodi ambayo kwao ni faraja kubwa mno,” alisema Lundenga.
Alisema pia kamati yake imegundua kwamba mashindano hayo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994 hadi mwaka huu ni miaka 18, ambayo washiriki watakaoshiriki wa mwaka huu wengi wao walikuwa wadogo wakati wakianza, hivyo anadhani imefika wakati sasa kwa serikali kuyatupia macho kwa kuwa wameonekana wasichana wengi  wananufaika na mashindano haya.
“Mashindano haya ya urembo pia yameonekana kuwa ya kimataifa zaidi kwa kuwa kuna baadhi yao wanafanya vyema katika mashindano ya kimataifa, akiwemo Happines Magesa, Tetemaria Malya, Flavian Matata, Miriam Odemba, Rehema Soud, Nelly Kamwelu  na Amanda Sululu,” alisema Lundenga.
Lundenga alisema kutokana na mwamko ulioonekana mwaka huu, kamati yake mwaka huu inataka kuyaboresha yaendelee kuwa na kiwango kikubwa zaidi  licha ya kwamba mashindano ya Miss Tanzania  yana mvuto na viwango vikubwa katika nchi za Afrika.
“Malengo yetu mwaka huu ni kuhakikisha tunapanua wigo mkubwa zaidi na kuyafanya kuendelea kuwa na nguvu zaidi katika nchi za Afrika zinazondaa mashindano ya urembo, licha ya kwamba mwaka 1995, Nancy Sumary kunyakua taji la Dunia Kanda ya Afrika  kwa kuingia fainali na kuwa miongoni mwa warembo  sita bora, ” alisema.
Aliwataja wanyange waliopata nafasi ya kushiriki fainali ya Miss Tanzania 2011 hadi sasa ni Chiaru Masonobo, Zerulia Manoko, Maua Kimambo, Dalila Gharib, Christine Mwenegoha, Christine William, Atu Daniel na Leyla Juma.
Wengine ni  Zubeda Seif, Stacey Alfred, Rose Hurbet, Husna Twalib, Cynthia Kimasha, Mwajab Juma, Neema Mtitu na Weirungu David.
Aliwataja wengine ni Loveness Flavian, Asha Saleh, Mariaclara Mathayo, Trace Sospeter, Irene Karubaga, Glory Samuel, Stella Mbuge, Husna Maulid na Hamisa Hussein.
Lundenga alisema washiriki wengine watatu kutoka Kanda ya Miss Ilala, watapatikana Ijumaa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, na kukamilisha idadi ya warembo 30 watakaoingia kambini.

Comments