WANALIZOMBE YAONDOA PINGAMIZI KWA SIMBA DHIDI YA ULIMBOKA

Klabu ya Majimaji ya Songea imeliandikia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikiondoa pingamizi ililoweka awali dhidi ya mchezaji Ulimboka Mwakingwe (pichani) ambaye Simba imemuombea usajili kwa msimu wa 2011/2012.
Majimaji kupitia Katibu Mkuu wake Henry Kabera imesema baada ya kukutana na uongozi wa Simba imeamua kuondoa pingamizi dhidi ya mchezaji huyo ambaye ilimsajili kwenye dirisha dogo msimu uliopita.
Awali Majimaji iliwasilisha pingamizi TFF  kwa wachezaji wake kumi na moja (11) iliosema kuna tetesi wamesajiliwa na klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom, lakini hawajafanyiwa uhamisho ingawa bado wana mikataba na timu hiyo.
Wachezaji hao ni Said Mohamed (Yanga), Ulimboka Mwakingwe (Simba), Ally Bilaly (Villa Squad). Pia wapo Juma Mpola (Kagera Sugar), Evarist Maganga (Villa Squad), Kulwa Mobby (Polisi Dodoma), Paul Ngalema (Ruvu Shooting), Mohamed Mpola, Lulanga Mapunda (Toto Africans), Hamad Waziri na Yahya Shaban Haruna.

Comments