SIMBA YAFUATA NYAYO ZA YANGA

SIMBA imefuata nyayo za Yanga kulilia mapato ya michuano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati '  KAGAME CUP'   .
Yanga ambao ni mabingwa wa michuano hiyo iliyomalizika nchini hivi karibuni walipeleka kilio chao kwa baraza la vyama vya soka katika ukanda huo (CECAFA) wakidai kutoshiriki kirahisi michuano hiyo mwakani mpaka pale yatakapofanyika marekebisho katika suala la mapato.
Yanga ilifikia hatua hiyo kutokana na kupata mgao wa Mil. 16 kati ya mil.354 zilizoingia aktika mechia yao ya fainali na Yanga kwenye uwanja wa taifa, jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa timu hizo wote wamelia kuumizwa na mapato hayo kutokana na ukweli kwamba wamekuwa wakiziandaa timu kwa gharama kubwa sana  na mwisho wa siku wanapata mafao kiduchu.          
     

Comments

  1. kuema kweli timu hizi zinanyonywa na vyama hivi si TFF na CECAFA haingii akilini timu zitumie kiasi kikubwa kuandaa timu siku ya siku wanaofaidika ni viongozi wa vyama hivi

    ReplyDelete

Post a Comment