SIMBA WERA WERA , YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME

WEKUNDU wa msimbazi, timu ya soka ya Simba imetinga nusu fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuikwanyua Bunawaya ya Uganda kwa mabao 2-1 katika mechi ya robo fainli iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba itakwaana na El Mereikh ya Sudan katika mechi ya nusu fainali mwishoni mwa wiki, ambapo El Mereikh ilikata tiketi hiyo baada kuifunga Ulinzi ya Kenya.

Comments

Post a Comment