SHIBOLI:NAJUUTA KUJIUNGA NA SIMBA...BORA NINGEKWENDA YANGA

NAJUUTA kujiunga Simba...ni maneno ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya soka ya Simba Ali Ahmed Shiboli (pichani kushoto)ambaye amedumu katika timu hiyo kwa miezi nane tu.
Shiboli, aliyesajiliwa na Simba kutoka klabu ya KMKM ya Zanzibar katika dirisha dogo la msimu wa ligi kuu bara msimu wa 2010/2011 kwa mkataba wa miaka mitatu, amedai kusikitishwa na kitendo cha kuondolewa katika timu hiyo nma kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera.
Alisema anasikitishwa na kitendo hicho kwani ni kama kumshuhshua hadhi yake kutokana na ukweli kwamba yeye anajiamini kuwa ni mchezaji bora lakini hakupata bahati ya kupangwa katika mechi za timu yake na hata chache alizopangwa alicheza kwa muda mfupi.
Mfungaji huyo bora mara mbili mfululizo wa ligi ya Zanzibar aliongeza kuwa, aliamua kujiunga na Simba kutokana na Mapenzi yake kwake kwa klabu hiyo na kuipiga kisogo Yanga ambayo pia ilikuwa ikimuwania lakini leo hii shukrani ya punda ni mateke.
"Najuta kujiunga na Simba ni bora ningekwenda Yanga nisingepotezwa kama ilivyo sasa, sintokuywa tayari tena kuichezea Simba hata iweje", Alisema Shiboli.

Comments