RUVU SHOOTING YAKARIBISHA MAOMBI YA UWANJA WAKE

KLABU ya soka ya Ruvu Shooting imezikaribisha timu zinazotarajiwa kushiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu ujao kuomba kutumia uwanja wake mpya uliopo Mlandizi Pwani.
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwiire amesema kwamba timu ambazo hazina viwanja zinakaribishwa kutuma maombi ya kutunmia uwanja huo kwani tayari maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walifanya ukaguzi wiki iliyopita na kuridhia kwa asilimia 90.
Alisema viongozi hao waliliridhia uwanja huo kutumika katika ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 20 huku wakitaka kukamilishwa kwa mambo madogo ambayo hata hivyo yatakamilika mpka kufikia Agosti 10 mwaka huu.

Comments