REDD'S MISS TEMEKE KUTEMBELWEA TBL KESHO

WANYANGE wanaowania taji la Redds Miss Temeke, leo(jnne) watatembelea makao makuu ya wadhamini wakuu wa kanda tatu za Dar es Salaam, kampuni ya bia nchini(TBL) ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya kumsaka mrithi wa Geneveive Mpangala.

Redds Miss Temeke ambayo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii, Jumamosi Julai 16 kwenye ukumbi wa TCC Changombe, iliywarembo 16 kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe watapanda jukwaani katika shindano hilo la kwanza katika kanda za Dar es Salaam.

Kwenye ziara hiyo ya leo itakayoanza mchana hadi jioni, warembo hao wataona na kuapata maelekezo jinsi ya vinywaji mbalimbali vinavyoetengenezwa kiwandani hapo ikiwamo na kinywaji cha Redd's ambacho kimedhamini shindano lao, ambapo baadaye jioni watajumuika na uongozi wa kampuni hiyo katika hafla fupi.

Taji la Miss Temeke 2010,Geneveive ambaye pia ni Miss Tanzania kupitia kanda hiyo, alikuwa mshindi wa Redds Miss Temeke mwaka jana alipopata tiketi ya kushiriki Miss Tanzania sanjari na washindi wengine wawili, Anna Daudi na Britney Urassa.

Wanyange wa mwaka huu ni pamoja na Cynthia Kimasha, Elizabeth Boniface, Eunice Mbuya, Husna Twalib, Irene Jackson, Joyce Maweda, Lucia John, Mwajuma Juma, Naifat Ally, Naomi Ngonya, Prisca Stephen,  Sasha Seti, Sara Said, Sara Paul na Victoria Mtega.

Mbali ya Geneveive, warembo wengine waliopata kutwaa taji la Miss Tanzania kupitia Temeke ni pamoja na Happiness Magesse 'Millen' (2001) na Sylvia Bahame mwaka 2003. Pia warembo Jokate Mwegelo aliwahi kutwaa taji la ubalozi wa Redds huku mwaka 2009, Sia Ndaskoy alishinda taji la ubalozi wa Utalii.

Mashindano ya Miss Temeke yalianza mwaka 1996 ambapo mshindi alikuwa mwandaaji wa Miss Shinyanga, Asela Magaka. Warembo wengine waliopata kutwaa taji la Miss Temeke ni pamoja na Khamisa Miriam Odemba(19997), Khamisa Ahmed(1998) na Ediltrda Kalikawe(1999).

Wengina ni  Irene Kiwia(2000) na  Happiness Magese 'Millen'(2001).Regina Mosha (2002), Slyvia Bahame(20030, Cecylia Assey(2004), Seba Agrey(2005), Jokate Mwegelo(2006), Queen David(2007), Angela Lubala(2008), Sia Ndaskoy(2009) na Genevive Mpangala anayeshikilia taji hilo.

Safari ya kuelekea Vodacom Miss Tanzania ambapo mshindi wa mwaka huu atakwenda London nchini Uingereza katika mashindano yatakayofanyika  Novemba 6, yatakayoambatana na sherehe za kutimiza miaka 60 ya mashindano ya urembo ya Dunia ambayo yalianza mwaka 1951.

Mbali ya kampuni ya bia nchini TBL kuwa wadhamini wakuu kupitia kinywaji chake cha Redds Original, wadhamini waliokwisha thibitsha hadi sasa ni Vodacom Tanzania ambao pia ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, gazeti la Jambo Leo na  saluni ya kisasa iliyopo katikati ya jiji ya Sally Salon. Kambi ya Miss Temeke ipo chini ya wakufunzi Carlo Zayumba na Anna Daud sanjari na Dickson Detram kwa upande wa shoo.
Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions         

Comments