MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI KUFANYIKA SEPTEMBA 24


Mtihani wa Uwakala wa Wachezaji wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) utafanyika Septemba 29 mwaka huu. Mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili;
maswali kutoka FIFA na kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
utafanyika saa 4 asubuhi.
 Kwa Watanzania wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wafike TFF ili waweze kupewa
taratibu za mtihani huo ambao ada yake ni dola 50 za Marekani.
 Wahusika wa mtihani huo ni wale wanaotaka uwakala kwa mara ya kwanza. Kwa wale
wenye leseni za uwakala wanatakiwa kuziuhisha (renew) kila baada ya miaka
mitano.
 Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA.
Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John
Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.
RHINO SPORTS YAUZWA MBEYA
Halmashauri ya Jiji la Mbeya (Mbeya City Council) imeinunua timu ya daraja la
kwanza ya Rhino Sports Club ya Arusha. Hivyo timu hiyo sasa makao makuu yake
yatakuwa Mbeya na itaitwa Mbeya City Council Sports Club- MCC.

Pia uongozi wa Halmashauri hiyo umemteua Kocha Juma Mwambusi kuwa Meneja wa timu
hiyo na amepewa idhini ya kushughulikia usajili na taratibu nyingine za ushiriki
wa MCC katika Ligi Daraja la Kwanza na mashindano mengine.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Comments