KIGOMA MABINGWA COPA COCA COLA

KIGOMA jana walitwaa ubingwa wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Copa Coca Cola kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam baada ya kuichapa Morogoro mabao 2-0.
Kwa ushindi huo, Kigoma wamepata Sh. Milioni 45.5, Kombe na Medali za Dhahabu, washindi wa pili Milioni 3, Kombe na Medali za Fedha na wa tatu Milioni 2, Kombe na Medali za Shaba.
Mabao ya mabingwa hao wapya, yote yalitiwa kimiani na Ismail Moba kwa kichwa dakika ya 24 na 59, kwa shuti kali. Katika mchezo wa utangulizi kusaka mshindi wa tatu, Temeke iliibuka mshindi kwa mikwaju ya penalti 4-2, kufuatia sare ya bila kufungana katika muda waq kawaida.
Katika michuano hiyo Miraj Suleiman wa Morogoro aliibuka mchezaji bora, refa bora Liston Hiari, kocha bora Ally Jangalu wa Morogoro, kipa bora Mwalo Ilunga wa Kigoma, wafungaji bora Godson Naftali wa Kigoma pamoja na Yunnus Moshi wa Mjini Magharibi, ambao wote kila mmoja alipata Sh. 500,000.

Comments