JITEGEMEE SEKONDARI YATINGA FAINALI MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS


Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya jijiji Dar es Salaam, jana ilitinga katika fainali ya michuano ya Airtel Rising Stars baada ya kuifunga Shule ya Msogola 1-0, katika mchezo mkali na wa kuzizimua uliocheza katika uwanja wa Karume katika nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo.
Katika mchezo huo, kila timu ilianza mchezo katika hali ya kumsoma mwenzake huku timu zikijiami zaidi kuliko kushambalia. Hata hivyo, baada ya dakika 15 za mchezo, Jitegemee walibadilika na kuanza kumiliki sehemu kubwa ya mchezo huku wakipeleka mashambulizi tele kwenye lango la wapinzani wao. Hata hivyo washambulizi wake wanabidi wajilaumu wao kwani walionekana kukosa umakini kwenye umaliziaji na hivyo kukosa mabao mengi ya wazi na hadi mwisho wa kipindi cha kwanza hakuna timu iliokuwa imepata bao.
Kwenye mwanzo wa kipindi cha pili, timu zote zilifanya mabadiliko ambapo kwa upande wa Msogola  Goodluck Mabiki alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Sevellin Aloyce na kwa upande wa Jitegemee Raidhin Hafidh na nafasi yake kuchukuliwa na Hamisi Njechele. Hata hivyo, Jitegemee ilibidi isubiri hadi dakika ya 83 ya mchezo kupata bao la ushindi baada Omar Selemani kuiandikia bao baada ya kuunganisha vizuri krosi kutoka kwa Hamisi Njechele. Baada ya bao, Jitegemee walionekana kucheza zaidi mchezo wa kujiamini na mpaka dakika ya mwisho, Jitegemee walitoka kifua mbele. Nusu fainali ya pili ya michuano hiyo inachezwa leo katika ya Mbande Sekondari na Kinyerezi Sekondari.
Kwa upande mwingine jijini Mwanza michuano hiyo iilianza hapo jumatano ambapo Shule ya Sekondari ya Nsumba iliifunga Mwanza Sekondari 1-0 na Buswelu Sekondari ikawafunga Taqwa 1-0. Fainali ya michuano hiyo kwa Mwanza itafanyika Jumamosi ya wiki hii.
Michuano ya Airtel Rising Stars ni maalum kwa vijana wa shule za sekondari walio na umri chini ya miaka 17 na imedhaniwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Klabu ya Manchester United ya Uingereza. Lengo ya michuano ni kutafuta vijana wenye vipaji na kuviendeleza ambapo wakati wa kila mechi, wataalamu wa mpira wa miguu uchangua wachezaji bora ambao wataunda timu ya kuwakilisha kila mkoa katika fainali ya michuano hiyo itakaofanyika Septemba mwaka huu. Kwenye finali hizo, wachezaji bora sita watachanguliwa na watapata fursa ya kuhudhuria kliniki maalum itakayoendeshwa na Klabu ya Manchester United.

Comments