JAHAZI, KANGA MOKO KUVUNJA JUNGU MORO

KUNDI la muziki wa taarabu nchini la Jahazi Modern Taarab linatarajiwa kufanya onyesho maalum kwa ajili ya kuukaribisha mwezi wa mtukufu usiku wa Julai 29 katika ukumbi Savoi, mjini Morogoro.

Mratibu wa onyesho hilo, Said Mdoe alisema lengo ni kuwapa raha mashabiki wa huko na hasa ikizingatiwa kuwa baada ya hapo mfungo wa ramadhani utabisha hodi.

Alisema ili kuongeza nakshi za onyesho hilo, pia kundi maarufu la unenguaji la Kanga Moja Ndembe ndembe nalo litasindikiza ambapo litamiliki jukwaa kwa mitindo tofauti ya unenguaji.
 Mdoe aliongeza kuwa, Jahazi linaloongozwa na Mzee Yusuf pamoja na burudani ya nyimbo zake murua zinazofanya vema katika medani ya muziki wa taarabu nchini, pia watawaonjesha mashabiki wa huko vionjo vyao vipya.
 “Wakazi wa Morogoro na maeneo jirani kaeni mkao wa kula kwani Jahazi na Kanga Moja wapo katika maandalizi ya nguvu ili kuhakikisha siku hiyo wanashusha burudani ya nguvu,”Alisema.

Comments