DJOKOVIC NDIO MAMBO YOTE KWENYE TENISI

Novak Djokovic ametwaa ubingwa wa tenisi wa Wimbledon na kushika namba moja kati chati ya wachezaji bora duniani na amesema yeye ni babu kubwa sasa.
Mserbia huyo mwenye umri wa miaka 24, amemfunga Rafael Nadal kwa seti 3-1, yaani 6-4, 6-1 na 6-3 na 1-6 na kujiwekea rekodi ya kushinda taji la tatu la Grand Slam.
Djokovic, ambaye alimbwaga Nadal katika namba moja ya wakali wa tenisi baada ya kushinda Nusu Fainali Ijumaa iliyopita, alisema: "Nimetimiza malengo yangu ya muda mrefu katika maisha, nimefanya ndoto zangu zimekuwa kweli ndani ya miaka mitatu.

Comments