BUNGE LAPONGEZA USHINDI WA YANGA

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa katika mashindano wa kombe la Kagame.
Pongezi hizo zilitolewa bungeni leo  na Spika Anne Makinda, alipokuwa akisoma matangazo mbalimbali baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Alisema ushindi wa timu ya Yanga katika michuano hiyo umeiletea heshima nchi.
“Kwa namna ya pekee kabisa, Bunge linaipongea timu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kagame,” alisema Spika Makinda alipokuwa akisoma moja ya matangazo hayo.
Alisema kutokana  na ushindi huo, wabunge Ismail Rage, Samuel Sitta, Juma Nkamia, Musa Zungu, Job Ndugai, Zitto Kabwe, Juma Kapuya, Iddi Azzan, William Ngeleja na Khalifa Khalifa, wamealikwa katika hafla ambayo haikulezwa itafanyika sehemu gani.
“Hili tangazo halijasema hafla hii itafanyika wapi, hivyo mlioalikwa mtapajua mkiwasiliana na aliyeandika tangazo hili,”alisema Spika.
Hata hivyo, alisema bunge linazopongeza timu za Yanga na Simba kwa kuingia fainali katika michuano hiyo, kwani zimeleta heshima kubwa kwa taifa kutokana na kulitwaa kombe hilo  mara 10.
“Timu ya Simba imetwaa kombe mara sita na Yanga limetwaa mara nne, hii ni heshima kubwa kwa taifa,” alisema.
 Pia aliwapongeza mashabiki wa timu zote mbili kwa kuonyesha ukomavu wakati wa mashindano hayo.

Comments

  1. mlikua hamjui anne makinda yanga damu toka akiwa msichana ndio maana hata mh.sitta akiwa spika walikua wakitupiana madongo simba na yanga zikicheza,hivyo tunaomjua hatukushangaa,yule yanga wa kulia machozi

    ReplyDelete

Post a Comment