BOBAN AMUONYESHA JEURI POULSEN

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya soka ya Simba ambaye haishiwi vituko kila kukicha, Haruna Moshi Boban amemuonyesha ujeuri alionao kocha mkuu wa timu ya soka ya Taifa 'Taifa Stars', Jan Poulsen.
Poulsen alimuita Boban, Juma Seif pamoja na Gaudance Mwaikimba katika kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 23 ili kuweza kuangalia viwango vyao kama ataweza kuwaita katika kikosi chake.
Hata hivyo, Boban anayesifika kwa utovu wa nidhamu uliokithiri ameshindwa kujiunga na kikosi cha vijana kilichopo mjini Arusha kikicheza mecghi za kirafiki na wenzao wa Shelisheli.
Hatua ya Boban ni muendelezo wa tabia yake mbaya ambayo amekuwa akisifika kuwa nayo kiasi cha kumfanya atimuliwe Stars na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Marcio Maximo.
Kama hiyo haitoshi, Boban pia alivunja mkataba wa kuichezea klabu ya Geffle IF ya Sweden na yote ilichangiwa na utovu wake wa nidhamu.

Comments

  1. Tulia kidogo Mkuu mchezo wenyewe unakwenda na umri halafu muda haugandi aisee!:-(

    ReplyDelete

Post a Comment