AZAM FC YAGOMA KWENDA NCHINI MALAWI



UONGOZI wa klabu ya Azam FC umefuta ziara ya kimichezo waliyokusudia kuifanya nchini Malawi kutokana na hali mbaya ya usalama iliyoko nchini humo kwa sasa.

Malawi imekumbwa na machafuko yanayodaiwa kusababishwa na hali ngumu ya maisha iliyosababishwa na kuporomoka kwa thamani ya fedha ya nchi hiyo.

Azam ilipanga kufanya ziara ya kimichezo nchini humo ikiwa ni maandalizi ya msimu mpaya wa ligi kuu uliopangwa kuanza Agosti 20 mwaka huu.

Comments