YANGA WAPATA SARE YA ZALI

YANGA jana ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa Kundi B michuano ya Castle Kagame Cup, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

El Mereikh ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya kwanza kupitia kwa Kelechi Osunwa, baada ya kuunganisha vema krosi ya Karim Eddafi, kabla ya Yanga kusawazisha dakika nne baadaye, baada ya beki wa El Mereikh, Ahmed Albasha kujifunga katika harakati za kuokoa. Yanga ilipata bao la pili dakika ya 30 baada ya mshambuliaji Mghana, Kenneth Asamoah kumlazimisha beki wa Merreikh Musab Omar kujifunga.
El Mereikh, walisawazisha bao dakika ya 63 baada ya Steven Worgu, kupiga shuti lilomshinda kipa Yaw BerkoKatika mchezo mwingin wa Kundi C uliofanyika katika Uwanja wa jamhuri Morogoro, mabingwa watetezi, APR ya Rwanda iliaanza vema baada ya kuitandika Port ya Djibout mabao 4-0
Katika mchezo wa Dar es Salaam timu zilipangwa hivi; Yanga: Yaw Berko, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Chacha Marwa, Nadir Haroub, Nurdin Bakari, Julius Mrope, Rashid Gumbo, Davies Mwape, Jerry Tegete/ Keneth Asamoah, Kigi Makassy.
EL Mereikh: Isam Elhadari, Saeed Mustafa, Badr Eldin, Ahmed Albasha, Nasr Eldin, Musab Omer, Kelechi Osunwa, Balla Gabar, Wawa Pascal, Karim Eddaffi, Remi Adiko.



Mshambuliaji wa Yanga Davies Mwape akiipasua ngome ya Merreikh

Comments