YANGA KUSAJILI KIFAA TOKA SWAZILAND

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga wako katika mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa klabu ya Mbabane Highlanders ya Swaziland, Mtanzania, Mohamed Suleimani aliyekuwa akikipiga katika klabu hiyo ambayo ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo.

Mshambuliaji huyo ambaye katika timu hiyo aliwahi kucheza ushambuliaji wa pembeni ambazo ni namba saba na 11.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema, mchezaji huyo ni raia wa Tanzania ambaye baada ya kumaliza ligi Kuu nchini humo hivi karibuni na kumaliza mkataba na timu yake amewasili nchini kwa ajili ya kusaka timu atakayochezea.
Sendeu alisema kwa kuwa wako katika mchakato wa kusaka kikosi cha Ligi Kuu Tanzania bara na Klabu bingwa Afrika, benchi la ufundi la Yanga litamuangalia mchezaji huyo kabla ya kumsajili.
“Tutamtazama mchezaji huyu kupitia benchi la ufundi, akionekana anafaa atasajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara,” alisema Sendeu.

Comments