WATOTO WA JULIO KUAGWA KESHO TAYARI KWENDA NIGERIA

Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ambayo Jumamosi (Juni 18 mwaka huu) itacheza ugenini na Nigeria katika mechi ya marudiano ya mchujo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani London, Uingereza itaagwa kesho.
U 23 itaagwa saa 7 mchana kambini F&J Hotel iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam.
Mechi dhidi ya Nigeria itachezwa Uwanja wa Samuel Obgemudia ulioko Benin City, ambapo ni kilometa 320 kutoka Jiji la Lagos.
Waamuzi wa mechi hiyo ambao wote wanatoka Senegal ni Ousmane Fall (mwamuzi wa kati), Maguette Ndiaye, Cheikh Toure na mwamuzi wa akiba Daouda Gueye. Kamishna ni Emmanuel Zombre kutoka Burkina Faso.

Boniface Wambura
Ofisa Habari

Comments