WASANII WA TANZANIA WAITWA KUSHIRIKI MAONYESHO NCHINI ITALIA

Baraza la Sanaa la Taifa kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.limepokea taarifa ya wasanii wa Tanzania kutakiwa kushiriki Maonyesho ya 16 ya sanaa ya Kimataifa yatakayofanyika Mjini Rho,Italia.

Maonyesho haya yanalenga bidhaa za asili na za kiutamaduni kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Asili (typical products) , Muziki (Musical events), Ngoma (Dances), Mapambo (colours) na vyakula (flavours) ambazo kwa ujumla wake zinaelezea historia ya nchi na watu wake.

Baraza linahimiza vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii, wadau wa sanaa  kutumia fursa hii kuonyesha kazi mbalimbali za sanaa katika Tamasha hilo hapo
juu.
Kwa maelezo  zaidi juu ya maonyesho haya, wasanii na wadau wa sanaa watembelee tovuti ya www.artigianoinfiera.it au kuwasiliana na waandaaji kupitia barua pepe cratfsfair@gestionefiere.com au kwa simu +39 02 31911911 au nukushi  +39 02 31911920.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI

Comments