WANACHAMA WA KLABU YA SIMBA WAOMBWA KUWA NA SUBIRA

UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba umewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa na subira katika kipindi hichi cha maandalizi ya timu yao.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa msigano baada ya timu ya Simba kuondoshwa kwenbye michuano ya kimataifa na Dc Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wiki iliyopita katika mchezo wa kuwania kucheza 16 bora ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kwa mujibu wa uongozi wa Simba kwa sasa wapo katika kukijenga kikosi chao ili kiweze kuonyesha matunda katika siku za usoni hivyo ni muhimu wanachama kushirikia na viongozi katika kuijenga timu.

Comments

  1. kufungwa ni sehemu ya matokeo na timu kucheza chini ya kiwango hutokea ndani ya mchezo. Ni muhimu simba watulizane waunde kikosi imara, na isitoshe mechi hizo mbili wamestushwa simba.
    www.aboodmsuni.blogspot.comkufungwa ni sehemu ya matokeo na timu kucheza chini ya kiwango hutokea ndani ya mchezo. Ni muhimu simba watulizane waunde kikosi imara, na isitoshe mechi hizo mbili wamestushwa simba.
    www.aboodmsuni.blogspot.com

    ReplyDelete

Post a Comment