USAIN BOLT AREJEA NA DHAHABU YAKE

BINGWA wa dunia wa mita 100 na 200 Usain Bolt raia wa Jamaica, jana alirejea kazini baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka, lakini akatwaa medali ya dhahabu katika mita 200, zilizofanyika Oslo, Norway.
Bolt mwenye miaka 24 ambaye alijiandikia rekodi kwa kutwaa medali tatu za Dhahabu katika michuano iliyopita ya Olimpiki, juzi alitumia sekunde 19.86 kumaliza mbio hizo.
Muda huo ni sekunde tano chini ya rekodi ya muda bora zaidi Duniani kwa mbio hizo aliyoiweka yeye mwenyewe na ile ya Frankie Fredericks, hata Bolt anasema akikaa sawa ataivunja rekodi hiyo.
Katika mbio za juzi Bolt aliongoza tangu mwanzo hadi mwisho akimuacha Jaysuma Saidy Ndure aliyeshika nafasi ya pili kwa sekunde 0.5, hata hivyo Bolt alielezea kufurahishwa na kasi aliyotumia kwa kuwa hajakimbia mita 200 tangu Mei mwaka jana aliposhiriki mbio za Shanghai, China.
“Kwa kuwa sijashiriki mbio kwa muda mrefu nadhani muda huu niliotumia sio mbaya, naona nimeanza vizuri, ila nijajifua zaidi naamini ninao uwezo wa kukimbia kwa kasi zaidi ya hivi,” alisema Bolt.
Bolt alisema anataka ashiriki mashindano matatu zaidi kabla ya kushiriki mbio za ubingwa wa Dunia zitakazofanyika Daegu, Korea Kusini, Agosti mwaka huu na kwamba kwa sasa atajifua sana chini ya Kocha weke Glen Mills.

Comments