UCHAGUZI MPIRA WA MEZA WADODA

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limehimiza wadau wa mpira wa meza nchini kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea uongozi wa nafasi mbalimbali katika chama cha mchezo huo.

Ofisa michezo mwandamizi wa BMT, Mohamed Kiganja, alisema kuwa hadi sasa wamejitokeza wagombea wawili ambao ni Felix Maganjira anayewania nafasi ya mwenyekiti na Abbas Mbonga anayewania nafasi ya katibu.
Nafasi zinazowaniwa ni pamoja na mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu, katibu msaidizi, mweka hazina na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Hata hivyo, uchaguzi huo ambao ulikuwa ufanyike Mei 24 kabla ya kuahirishwa kutokana na watu kutojitokeza kuwania, utafanyika katika tarehe itakayopangwa baadaye.

Comments