TIMU 16 KUWANIA 'KAZI SHERIA CUP'TIMU 16


TIMU 16 za soka toka sehemu mbalimbali zinatarajiwa kushiriki mashindano ya soka yaliyobatizwa kwa jina la ‘Kazi Sheria Cup’ yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 17 katika uwanja wa CCM Msasani (Magunia), jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa michuano hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Popular Sports & Entertainment Tanzania, Badili Mangula amesema kwamba lengo la kutoa fursa kwa vijana toka sehemu mbalimbali kuonesha vipaji vyao hivyo kuweza kusajiliwa katika timu zinazoshiriki ligi mbalimbali.

“Pamoja na burudani ni muda muafaka wa kutumia kipindi hiki cvha mapumziko ya ligi kutoa fursa kwa wadau wa michezo kuhudhuria mashindano kama haya na kujiona vipaji tofauti”, Alisema
 Aliongeza kuwa mashindano hayo ambayo ni ya kipekee kuliko yote ya mchangani yaliyowahi kufanyika ndani ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kuwepo kwa zawadi ambazo washindi hawajawahi kupewa.
 Alisema bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa fedha taslim shilingi mil.1.1 pamoja na kikombe, mshindi wa pili atazawadiwa shilingi 500,000, huku mfungaji bora atazawadiwa sh.50,000 ambapo michuano hiyo imedhaminiwa na benki ya Diamond Trust na Sunda International.
 Timu zitakazoshiriki ni pamoja na Kisiwani, Orphans, Nyara, Masaki United, Makamba Jeki, CCBRT, Makangira, Simple Camp, Polisi, Tutambuane, Wabishi, Mkungu Pesa, Samaki Samaki, Chevo, KKKT FC na Bongo Msoto.

Comments