TETEMEKO LATIKISA MIJI YA DSM, ZNZ, TANGA

TAFRANI ilitokea mchana wa leo katika jiji la Dar es Salaam na hasa kwa watu waliopo katika majengo marefu kufuatia tetemeko la ardhi lililojitokeza kwa sekunde kadhaa kabla ya kutoweka..

Wakazi wa majengo hayo walionekana kutoka nje kwa ajili ya kuhofia usalama wao kabla ya kurejea baada ya hali kuwa ya kawaida.
Wataalamu wa hali ya hewa wamasema tetemeko hilo lilitokea kilometa 52 kusini mashariki mwa jiji  lilikuwa na nguvu ya 4.8 upana km 10, huku pia maeneo ya  Zanzibar, Tanga na Nairobi nchini Kenya nayo yalikumbwa na rabsha hiyo.

Comments