TANZANIA FIRST ANNUAL CHARITY MASQUERADE BALL!

 MBUNIFU WA MAVAZI NCHINI JAMILA VERA SWAI KUSHOTO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO KUHUSINA ANA ONYESHO MAALUM LA KUCHANGISHA FEDHA ZA KUWAWEZESHA WENYE MATATIZO YA MACHO NCHINI 'MASQUERADE BALL CHARITY', KATIKATI NI MWENYEKITI WA DAR LIONS CLUB HOST FRANK GOYAYI  NA KULIA NI BALOZI WA FASHION 4 VISION, FAREED KUBANDA MAARUFU KAMA FID Q.


 FID Q AKITOA NENO KWA WANAHABARI HUKU AKISIKIIZWA KWA UMAKINI NA MENEJA MASOKO NA MAWASILIANO WA BENKI YA EXIM, LINDA CHIZA AMBAPO BENKI HIYO NI MOJA YA WADHAMINI WA TUKIO HILO.

ONYESHO maalum la mavazi kwa ajili ya kuchangia watu wenye matatizo ya macho nchini linalokwenda kwa jina la 'Lions club annual masquerade ball' linatarajiwa kufanyika Juni 11 katika hoteli ya Kilimanjari Kempisk jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika ukumbi wa Club Bilicanas, Mwenyekiti wa Lions Club Dar Host ya jijini Dar es Salaam Frank Goyayi alisema lengo la kuandaa onyesho hilo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya wahitaji chini ya programu ijulikanayo kama macho kwanza.
"Hafla hii si kwa ajili ya kuchangia kunusuru macho ya watanzania tu, bali pia itakua ni tukio la kuwaleta pamoja viongozi wote wa Tanzania katika ngazi mbali mbali chini ya mwamvuli mmoja kwa nia moja ya kutumikia watu wenye mahitaji ya kujitibu machjo yao", Alisema
Kwa upande wake balozi wa fashion 4 Vision ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Fareed Kubanda 'Fid Q' anawajibika kutoa mchango wake kwa watu wenye uhitaji wa matibabu ya macho kupitia usanii wake, hivyo ataendelea na jitihada zake za kuhakikisha ujumbe unawafikia watu wengi kupitia muziki.

Onyesho hilo la Fashion 4 Vision Annual Masquerade Ball ambalo kiingilio chake kitakuwa sh.100,000 limedhaminiwa na Exim Bank, kwa kushirikiana na Club Billicanas, Coca cola, Global Outdoor Systems, 2M Media, Lotus Creative Concepts, Choice Fm , Clouds TV, Fashion 4 Health, Daily news, Habari Leo, Oman Air na 361 Degrees.

Comments