SIMBA WAREJEA JIJINI TAYARI KUWAKABNILI WACONGOMAN

WEKUNDU wa msimbazi timu ya soka ya Simba imerejea jijini leo kutoka mjini Tanga ilipokwenda kuweka kambi maalum ya kujiandaa na mechi yake ya kuwania kucheza 16 bora ya michuano ya shirikisho la soka barani Afrika dhidi ya Dc Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Simba Mganda Moses Basena amesema kwamba hana wasiwasi na mechi hiyo kutokana na ukweli kwamba anawafahamu vilivyo Wacongo hao na tayari amewapa mbinu kadhaa wachezaji wake ili kuweza kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.

Comments

  1. kazi kwenu wachezaji, sio ushabiki kwa saana na kuwatia moyo, lakini mwisho wa siku inakula kwenu...mpira sasa ni ajira. TWAWATAKIA MAFANIKIO MEMA

    ReplyDelete

Post a Comment