SIMBA V YANGA VETERAN KUKIPIGA KESHO MJINI IRINGA

                                                                             SIMBA VETERANS
YANGA VETERANS

MAVETERANI wa timu za soka za Simba na Yanga All Stars kesho watacheza
mechi ya kirafiki itakayofanyika kwenye Uwanja wa Samora uliopo Mjini Iringa.
Mratibu wa mechi hiyo, Ally Mduba, alisema kuwa pambano hilo ni maalum kwa wakazi wa Iringa ambao hawajawahi kuona watani hao wa jadi wakichuana.
Mduba alisema wameamua kuzipeleka timu hizo mkoani humo ili kutoa nafasi kwa wakazi wa Iringa kushuhudia wachezaji hao ambao waliwahi kuvuma katika miaka ya 90.
Alisema mchezo huo utaanza majira saa 10:30 ya alasiri maandalizi yote yamekamilika.
Vikosi vya timu hizo vimeshawasili mkoani humo kwa ajili ya mchezo huo.
Kikosi cha Yanga kinaundwa na Kipa Peter Manyika, Bakari Malima, Edibily Lunyamila, Idd Moshi, Salvatory Edward, Omary Kapilima, Ephrahim Makoye, Ben Mwalala na Ally Yusuph Tigana.
Kikosi cha Simba kina wachezaji Issa Manofu,Thomas Kipese, Boniface Pawasa, Madaraka Suleiman, Shekhan Rashid, Edwin Mukenya, Suleiman Matola, Yusuph Macho, na Said Swed.

Comments