SIMBA SC YAZINDUKA KOMBE LA KAGAME

SIMBA leo imeanza kuonyesha matumaini ya kuwania kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame baada ya kuwafunga vinara wa kundi lao, Ocean View ya zanzibar kwa bao 1-0 katika mechi iliyopogwa kwenye uwanja wa Taifa.
Hata hivyo Simba ambayo ushindi huo umeifanya kuwa na pointi tatu sawa na timu Vital'O ya wanayo nafasi ya kutinga hatua hiyo iwapo watashinda mechi zao mbili zilizosalia.
Simba ambayo ilianza michuano hiyo kwa kutoka suluhu ya 0-0 na Vital'O wamebakiza mechi yao baina na Red Sea na Enticellers ambapo Ocean View inaongoza kundi lao kwa kuwa na pointi sita huku tayari ikiwa imeshakata tiketi ya robo fainali.

Comments