SIMBA KWENDA DRC ALHAMIS, KURUDIANA NA MOTEMA PEMBE JUNI 18

TIMU ya soka ya Simba inatarajiwa kuiondoka nchini keshokutwa (Alhamis) kwenda nchini KOngo kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya  DC Motema Pembe ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC),ikiwa ni mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya 16 ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF).
 Mchezo huo unatarajia kuchezwa jumamosi hii ya Juni 18 , katika mji wa Kinshasa  nai Simba inaendelea na maandalizi ya mechi hiyo baada ya kuifunga Motema Pembe bao 1-0 jumapili iliyopita katika dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam.

Comments