SIMBA KUEENMDELEZA UBABE KWA OCEAN VIEW KESHO?

KIKOSI CHA SIMBA
WEKUNDU wa msimbazi, timu ya soka ya Simbna wameapa kuendeleza ubabe kwa wakali wa Zanzibar, timu ya Zanzibar Ocean View kupitia mechi yao ya kuwania kombe la Kagame itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha mkuu wa Simba Mganda, Moses Basena amesema amekifanyia marekebisho kikosi chake ambacho kil;ianza michuano hiyo kwa kutoka suluhu ya bila kufungana na Vital' O ya Burundi, jumamosi iliyopita.
Hata hivyo, kocha wa Mmisri Abdulfatah Abass, ametuma salamu kwa wekundu hao na kusema kuwa kulipiza kisasi ni haki yao hivyo ni haki yao kufanya hivyo.
Kocha huyo ametoa kauli hiyo baada ya Simba kuifunga walipokutana Visiwani Zanzibar mapema mwaka huu.
Tayari Ocean View imeshajihakikishia klucheza robo fainali katika kundi lao naada ya kuwa na  pointi sita baada ya kucheza mara mbili ,huku simba ikihitaji pointi tatu muhimu ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutinga robo fainali, lakini jambo hilo halitegemewi kuwa rahisi, kwani Ocean View wameonyesha ustawi mkubwa tangu kuanza michuano hii.

Comments