SIMBA, DC MOTEMA PEMBE KAZI NZITO UWANJA WA TAIFA KESHO

                                                      SIMBA SC

DC MOTEMA PEMBE
WEKUNDU wa msimbazi timu ya soka ya Simba kesho inashuka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kukwana na Dc Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika mechi ya kombe la Shirikisho.

Wakizungumzia mechi hiyo makocha wa timu hizo kila mmoja amejinasibu kuibuka na ushindi hii leo ili kujiweka katika mazingira mazuri.
Kocha mkuu wa Simba, Mganda Moses Basena amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu na yenye upinzani mkubwa lakini watahakikisha wanashinda ili kujiwekea mazingira mazuri katika mechi ya marudiano.
Alisema kuwa,anafahamu wapinzani wao wana kasi sana hivyo amewataka wachezaji wake wote kucheza kwa ushirikiano badala ya kuwategea mabeki na kipa kwani watakapopoteza mchezo huo doa litakuwa la wote.
“Wenzetu wana kasi sana hivyo nawaomba wachezaji kuacha kutegeana, washambuliaji wasiachie mabeki kuzuia mpira...wote mshirikiane katika kudhibiti mashambulizi, kulinda goli na hatimaye kufunga magoli”, Alisema.
KOcha wa Motema Pembe, Andy Fopila amesema Simba ni kama uchochoro kwao.

Comments