ROSE MSUYA NDIYE MISS DAR INTER COLLEGE 2011

 MISS DAR INTER COLLEGE ROSE MSUYA (KATI) AKIPOZI KATIKA PICHA NA MSHINDI WA PILI BLESSING NGOWI KUSHOTO NA GLORIA PETER ALIYEKUWA WA TATU KATIKA SHINDANO LILILOFANYIKA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA UKUMBI WA SUNSIRO
 TOP FIVE
                                              ROSE JOHN AMBAYE ALIKUWA ANAVUA TAJI
                                                            MMOJA YA MAJAJI, MAMAPIPIRO
                MMOJA YA WASHIRIKI, GLORY PETER AKIPITA NA VAZI LA UBUNIFU
                             UNCLE HASHIM AKIBADILISHANA NAMBA NA DULLY SYKES
                                                                      BAADHI YA MASHABIKI
                                                                          MASHABIKI
                    DINA, NA HIDAN RICCO TOKA KAMATI YA MISS TANZANIA TULIKUWA MAJAJI
                                                                         KIKAZI ZAIDI
                                                             UMAKINI.COM
                 UNCLE MAKOYE AKIMKABIDHI ZAWADI MSHINDI WA TANO
                                              PRINCE DULLY SYKES AKIKAMUA
 MMOJA YA WADAU MAARUFU WA CLUB YA SIMBA HASSAN OTHMAN HASSANOO ALIKUWEPO NDANI YA NYUMBA, PIA ALIKUWA MMOJA YA WADHAMINI.

 
MWANAFUNZI kutoka chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Rose Msuya usiku wa kuamkia leo alifanikiwa kutwaa taji la Miss Dar Inter College mwaka 2011, katika shindano lilifanyika katika ukumbi wa Sunciro, Sinza jijini Dar es Salaam.
Rose alitwaa taji hilo lililokuwa linashikiliwa na Rose John wa Chuo cha Ustawi wa jamii, baada ya kuwashinda washiriki wenzake 14 waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka vyuo vya Cbe, Dsj, Ustawi wa Jamii na Ifm.
Mrembo Blessing Ngowi kutoka Chuo cha ustawi wa jamii ambaye alikuwa akionyesha upinzani mkali wa mshindi aliweza kushika nafasi ya pili huku, Gloria Peter wa Ifm alishika nafasi ya tatu.
Nafasi ya nne ilikwenda kwa Elizabeth Aloyce wa Chuo cha Ustawi, huku Winfrida William wa Cbe alishika nafasi ya tano katika shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Kapito Letaz ya jijini Dar es Salaam.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes alipamba shoo hiyo kwa burudani safi ambapo aliweza kuwarusha mashabiki kibao waliojitokeza ukumbini hapo kwa kupiga vibao vyake vikiwemo Handsome, Hi, Baby Candy, Salome, Shikide, Hunifahamu na ule unaotamba sasa wa Bongo Fleva.
Shindano hilo lilidhaminiwa na Vodacom, Redd's, Paris Pub, Brake Point Bar, Ndege Insurance, Clouds Media, Hassan Hassanoo, Januari Makamba, Zinduka, pamoja na blogu za mamapipiro, michuzi, mtaa kwa mtaa na fullshangwe.

Comments