AKUDO IMPACT BADO TUPO NA TUTAENDELEA KUWEPO

RAIS WA AKUDO IMPACT, CHRISTIAN BELLA NA ZAGREB

                                                          TOTOO ZE BINGWA NA BELLA
KIONGOZI AKUDO, PATRICK BUYANZI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO,ANAYEFUATA NI ZAGREB NA TARCIS MASELA
Na Dina Ismail


BENDI ya muziki wa dansi nchini Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ imesema bado ipo hai na kimya chake kina mshindo.
Rais wa bendi hiyo Christian Bella, alisema kwamba taarifa zinazotolewa kuhusiana na wasanii wa bendi hiyo kunyakuliwa na bendi nyingine ni za kizushi,na zina lengo la kuwaua kisanii.
Alisema wanaovumisha taarifa hizo ni wale wasioitakia mema, sambamba na kuihofia bendi yao kutokana na ubora iliyonayo katika kila idara ndiyo maana wameamua kuwavuruga kwa kutoa taarifa za uongo.
“Eti Maresa (Tarcis), Totoo ze Bingwa, Zegrab wamehamia bendi nyingine, huo ni uzushi usiokuwa na maana hawa tupo nao kama unavyoona nawaomba mashabiki mzipuuze taarifa hizo tupo kamili na muda si mrefu mtaanza kuona kazi zetu”, Alisema.
Aliongeza kwamba, wameamua kukaa kimya kutokana na albamu yao ya kwanza ‘Impact’ kuwa bado inafanya vizuri, hivyo wapinzani wao wametumia fursa ya kimya chao kutanga kuwa wamesambaratika ili wapate wasaa wa kazi zao kupata nafasi katika vyombo vya habari”, Alisema.
Bella alisema kwa sasa wapo katika maandalizi ya uzinduzi wa albamu yao ya pili iitwayo ‘History no Change’ iliyo na vibao kama Umejificha Wapi, Pongezi kwa Wanaondoa, Ubinafsi, Umefulia, Usikate tamaa, Ubinadam Kazi na Usifuate Wambeya.

Comments