POULSEN KUTETA NA MAKOCHA

                                         JAN POULSEN, KOCHA MKUU WA TAIFA STARS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Juni 15, 2011
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Sunday Kayuni watakutana na makocha 32 wa klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza. Mkutano huo utafanyika Juni 20 mwaka huu Ofisi za TFF kuanzia saa 3 asubuhi.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo ni maalumu kwa Poulsen kueleza falsafa yake ya ufundishaji, tathmini ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyomalizika Aprili mwaka huu, kutoa leseni za daraja A za ukocha za TFF kwa makocha husika na kubadilishana uzoefu.

Makocha husika wanatakiwa kugharamiwa na klabu zao kwa ajili ya kushiriki mkutano huo muhimu. TFF itagharamia chai na chakula cha mchana pekee.
Klabu za Ligi Kuu ni African Lyon, Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Moro United, Mtibwa Sugar, Oljoro JKT, Polisi Tanzania, Ruvu Shooting, Simba, Toto Africans, Villa Squad na Yanga.

Boniface Wambura
Ofisa Habari

Comments