POLISI WALISHUSHA JUKWAANI KUNDI LA MAPACHA WATATU



Na Martin Malera, Dodoma
POLISI mkoani hapa, juzi wamevunja onyesho la muziki wa dansi la Mapacha Watatu kwa madai kuwa hawakuwa na kibali kufanya onyesho hilo.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa sita kwenye ukumbi wa Kilimani mjini hapa, ambapo wasanii wa kundi hilo, Kalala Juniour, Halid Chokora na Jose Mara, walikatiza show yao baada ya askari kupanda jukwaani na kuwataka wavunje onyesho.
Hali hiyo iliibua tafrani kubwa kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa bendi hiyo waliokuwa na hasira ya kupoteza pesa zao.
Wapo mashabiki waliolewa ambao walilazimika kurusha viti na chupa jukwaani kwa polisi hao wakitaka Mapacha Watatu waendelee kutoa burudani.

Comments