OCEAN VIEW WATANGULIA ROBO FAINALI

ZANZIBAR Ocean View mchana huu wameshinda mabao 2-0 dhidi ya Red Star ya Eritrea katika mechi ya Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Castle Kagame kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hivyo kujiwekea matumaini ya kutinga Robo Fainali katika kundi hilo, lenye timu za Enticelles, Vital'O na Simba Sc pia.
Ushindi huo, umeifanya Ocean itimize pointi sita baada ya mechi zake mbili, mabao matano ya kufunga, mawili ya kufungwa na inafuatiwa na Vital'O yenye pointi nne na Simba zenye pointi moja kila moja, Red Sea na Enticelles ambao hawana pointi.
Katika mchezo wa pili wa kundi hilo, jana Vital'O ya Burundi iliizidi kuiweka pagumu Enticelles ya Rwanda baada ya kuifunga mabao 3-1, kwenye Uwanja huo huo Taifa, Dar es Salaam.

Comments

Post a Comment