NJOONI MUWAONE VIJANA WETU V NIGERIA KWA BUKU

Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itafanyika Jumapili (Juni 5, 2011) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili jioni.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 1,000 kwa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange straight and curve), sh. 5,000 kwa VIP C na B na sh. 10,000 kwa VIP A. Tiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2 asubuhi kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, Bigbon Msimbazi (Kariakoo), Steers (Mtaa wa Ohio na Samora), Uwanja wa Uhuru, Ubungo OilCom na vituo vya mauzo vya Premier Sports Betting.
Boniface Wambura
Ofisa Habari

Comments