NGASA KUWAKABILI MANCHESTER UNITED


MWENYEKITI WA AZAM FC MOHAMMED SAID AKIZUNGUMZA  NA WANAHABARI, KULIA NI MAKAMU MWENYEKIT WA SEATTLE SOUNDERS, LANCE LOPEZ
MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Azam Fc anatarajiwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kufanya mazoezi na Seattle Sounders ya huko ambapo uwepo wake huko anatarajiwa kuichezea timu hiyo dhidi ya Manchester United ya Uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Seattle Sounders Lance Lopes, alisema mazoezi hayo ya wiki mbili ambapo Ngassa ataondoka nchini kati ya Julai 6 na 7.
Alisema, Ngasa ambaye anakwenda huko kama sehemu ya kukuza na kuendeleza ushirikiano baina ya timu za Tanzania na timu yao kwa kipindi hicho atanapata wasaa wa kukutanana na Manchester ambayo itakwenda huko na wao wakiwa kama wenyeji.
Naye Mwenyekiti wa Azam Fc Said Mohammed alisema wanafurahi kwa hatua ya mchezaji wao kupata bnafasi hiyo kwani atakuwa Mtanzania wa Kwanza kuichezea timu inayocheza na Manchestyer United.
Alisema, timu yao ipo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vijana hivyo hatua hiyo ni moja katika mechi ya kirafiki baina yao na sehemu ya kumtangaza mchezaji katika sehemu nyingine duniani hivyo wamefurahishwa na mwaliko huo
Aliongeza kuwa, klabu yao haina pingamizi kwa mchezaji yoyote ambaye atahitajiwa kwenda nje ya nchi iwe kwa majaribio ama kucheza soka la kulipwa hivyo milangi ipo wazi kwa mtu yoyote kuwasaidia wachezaji wao katika kupata timu za nje ya nchi.

"Azam tupo katika kuendeleza soka, hivyo hatua ya Ngasa ni sehemu ya maendeleo yake kwani huwezi jua anaweza kuonekana na timu yoyote na kuvutiwa naye na kumnunua", Aliongeza.

Comments