ASANTE KOTOKO, HEARTS OF OAK ZAJA KUKIPIGA NA SIMBA, YANGA





NA Dina Ismail
TIMU za soka za Simba na Yanga zinatarajiwa kuungana na timu za Asante Kotoko na Hearts Of Oak kutoka Ghana kwa ajili ya kushiriki mashindano maalum ya kimataifa ‘Tanzania International Cup’ yatakayofanyika julai 16 na 17 katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,mkurugenzi mtendaji wa Lumuli Marketin inayoratibu michuano hiyo, Sidwell Jan alisema lengo la michuano hiyo ni kuwapa uzoefu wa kimataifa wachezaji husika.
Alisema kupituia michuano hiyo, klabu zitapata nafasi ya kuonyesha mbinu zao za mchezo wa soka, pia kuwapa uzoefu sambamba na kuongeza ushirikiano baina yao.
“Michuano hii itakuwa ikifanyika kila mwaka ambapo watakuwa wanazialika timu zenye historia kwenye soka barani Afrika hivyo klabu za Tanzania zinawqeza kunufaika na kupata uzoefu zaidi kwa kucheza na nchi zenye kiwango cha juu barani Afrika”, Alisema.
Aliongeza kuwa kupitia michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini, makocha wa timu shiriki watapata fursa ya kubadilishanauzoefu huku kukiwapo na mpango endelevu kwa kushirikisha klabu bingwa za soka barani Afrika.
Akizungumzia juu ya ushiriki wao, makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema ni michuano ambayo iatasaidia kuwaongezea ujuzi wachezaji wa timu za hapa nchini.
“Tunafurahi kushirikishwa katika michuano hii na tunaomba dua nyingi ili tupate nafasi ya kukutana na mahasimu wetu Yanga katika moja ya mchezo”, Alisema.
Naye mmoja ya wajumbe wa kamati ya fedha na uchumi ya Yanga, Isaac Mazwile alisema klabu yake imesajili wachezaji wazuri hivyo kupitia michuano wataleta changamoto kwa timu pinzani.
Pamoja na michuano hiyo ambayo viingilio vimepangwa kuwa dola 10,000 kwa kila mtu, kutakuwa na burudani mbalimbali , huku kituo cha televisheni cha TBC 1, na TBC Taifa vitarusha matangazo hayo.

Comments