MISS WORLD 2011KUFANYIKA NOVEMBA 9, UINGEREZA

Mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2011 yamepangwa kufanyika mjini London, Uingereza, Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga (pichani kushoto) amesema.

Lundenga amesema leo kwamba mashindano hayo yatafanyika Novemba 6 na warembo wanatakiwa kuingia London Oktoba 19 na kuanza kambi rasmi.
Alisema kuwa kutokana na kuwa tarehe hiyo, mshindi wa mwaka huu wa Vodacom Miss Tanzania atapata muda mrefu wa kujiandaa na mashindano hiyo ili kufanya vyema kama ilivyokuwa kwa Nancy Sumari mwaka 2005 alipoingia katika tano bora.
“Tumepokea taarifa kutoka kwa waandaaji wa Miss World kuhusiana na fainali za mwaka huu, muda ni mzri ambao utatupa fursa kubwa ya kufanya vyema katika kinyang’anyiro hicho,” alisema Lundenga.
Aliongeza kuwa kwa sasa wapo busy na mashindano ya ngazi ya vituo, wilaya na mikoa ambapo wanatarajia kufikia tamati mwezi ujao kabla ya kuanza kwa mashindano ya kanda na baadaye fainali za taifa.
Alifafanua kuwa wamejipanga kufanya shuguli nyingi za jamii ili kuweza kutimiza kipengele cha kazi za jamii au beauty with purpose.

Comments